KUFUATIA madai ya hivi karibuni ya mkongwe wa
filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ kuwa baadhi ya waigizaji hawana sifa
za kuwa wacheza sinema zaidi ya kuuza sura, msanii Yusuph Mlela amempa
dongo zito akisema licha ya umri kuwa mkubwa, pia ana matatizo flani
yanayomsumbua.

Msanii wa filamu Bongo, Yusuph Mlela.
“Nora naona siyo kosa lake kwani alishaugua yule, isitoshe
ameshakuwa bibi hivyo nimemsamehe na sina tatizo naye kwani najua,
lingekuwa jambo la maana kama angetufuata na kutushauri kama mkongwe
lakini si kwa njia aliyofanya,” alisema Mlela.

Mkongwe wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’
Hivi karibuni Nora aliwataja mastaa wenzake wa filamu akiwemo Mlela,
Chuchu Hans, Steve Nyerere, Kajala na Batuli akisema hawawezi kazi zaidi
ya kuuza sura tu.
No comments:
Post a Comment