Tuesday, 23 September 2014

CAPITAL ONE CUP: ‘WATAKATIFU’ WAITAKATISHA ARSENAL EMIRATES, LIVERPOOL YAITOA BORO MATUTA 14-13!

CAPITAL ONE CUP – RAUNDI YA TATU
MATOKEO:
Jumanne Septemba 23
Arsenal 1 Southampton 2
Cardiff 0 Bournemouth 3
Derby 2 Reading 0
Leyton Orient 0 Sheffield United 1
Liverpool 1 Middlesbrough 1 [Baada ya Dakika 120, 2-2, Penati 14-13]
MK Dons 2 Bradford 0
Shrewsbury 1 Norwich 0
Sunderland 1 Stoke 2
Swansea 3 Everton 0
Fulham 2 Doncaster 1
+++++++++++++++++++++++
ARSENAL 1 SOUTHAMPTON 2
CAPITAL_ONE_CUP-BESTWakiwa kwao Emirates, Arsenal wametupwa nje ya Kombe la Ligi, CAPITAL ONE CUP, na Southampton iliyotoka nyuma kwa Bao 1-0 na kushinda 2-1.
Alexis Sanchez alitangulia kuipa Bao Arsenal Dakika ya 14 kwa frikiki safi na Southampton walisawazisha baada ya Tomas Rosicky kumwangusha Sadio Mane na Dusan Tadic kufunga Penati hiyo katika Dakika ya 20.
Southampton walipata Bao lao la Pili Dakika ya 40 wakati Fulbeki wao wa Kulia Nathaniel Clyne alipounasa Mpira wa Kona uliokolewa akiwa Mita 35 na kuachia Shuti lililotinga wavuni.
Hadi mwisho Arsenal 1 Southampton 2.
VIKOSI:
Arsenal: Ospina, Bellerin, Chambers, Hayden, Coquelin, Rosicky, Diaby, Wilshere, Alexis, Campbell, Podolski
Akiba: Gibbs, Mertesacker, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Martinez, Ajayi, Akpom
Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Gardos, Targett, Wanyama, Schneiderlin, S. Davis, Tadic, Mane, Pelle
Akiba: Davis, Long, Cork, Bertrand, Mayuka, Reed, McCarthy
Refa: Keith Stroud
+++++++++++++++++++++++
LIVERPOOL 2 MIDDLESBROUGH 2
Hadi Dakika 90, Mechi hii iliyochezwa Anfield ilimalizika Bao 1-1 na kwenda Dakika za Nyongeza 30 ambazo Liverpool walipata ushindi wa Bao 2-1 kwa Bao la Dakika ya 109.
Liverpool walifunga Bao lao katika Dakika ya 10 baada ya Kipa wa Boro, Jamal Blackman, kuokoa Shuti la Rickie Lambert na Mpira kutua kwa Kijana wa Miaka 17, Jordan Rossiter, akiwa Mita 30 toka Golini na kupiga Shuti lililotinga wavuni.
Hadi Mapumziko Liverpool 1 Boro 0.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 62, Adam Reach aliisawazishia Boro kwa Bao laini la Kichwa.
Hadi Dakika 90, ngoma ilikuwa Sare ya 1-1 na Dakika za Nyongeza 30 zikaendelea na Liverpool kufunga Bao la Pili katika Dakika ya 109 kupitia Jesus Fernandez Suso.
Hata hivyo, katika Dakika ya 123, Raheem Sterling alifanya kosa kubwa kwa kutaka kuwarudishia Mabeki wake Mpira ambao ulinaswa na Bamford alieingia ndani ya Boksi na kuangshwa na Touré na Refa Jones kutoa Penati iliyofungwa na Bamford na Gemu kuwa 2-2.
Ikafuatia Tombola ya Mikwaju ya Penati ambazo Liverpool walikosa moja ile ya Raheem Sterling na Boro moja, iliyopigwa na Bamford, na Wachezaji waliobakia wote kupiga Penati, pamoja na Makipa wao na kufunga na Gemu kuwa Penati 10-10.
Ndipo Wachezaji wakarudia tena kupiga ambapo Balotelli aliifungia tena Liverpool na Bamford kufunga safari hii baada ya kukosa ya kwanza na kuendelea hadi Liverpool wakiongoza Penati 14-13 ndipo Albert Adomah alipopiga nje na kuwapa ushindi Liverpool kwa Penati 14-13.
VIKOSI:
Liverpool: Mignolet; Toure, Enrique, Sakho, Manquillo; Lucas, Rossiter, Lallana: Markovic, Sterling, Lambert.
Akiba: Jones, Moreno, Borini, Fernández Saez, Skrtel,  Balotelli, Williams
Middlesbrough: Blackman; Fredericks, Ayala, Omeruo, Friend; Adomah, Leadbitter, Clayton, Reach; Tomlin, Kike.
Akiba: Gibson, Konstantopoulos, Husband, Vossen, Bamford, Nsue Lopez , Wildschut

No comments:

Post a Comment