Tuesday, 23 September 2014

Ali Kiba anapendwa zaidi Uingereza kuliko Diamond?

Mabishano ya mashabiki kuhusu ni nani mkali kati ya Diamond na Ali Kiba ulionekana kufifia kwa muda kidogo kwenye media lakini ukweli ni kwamba pressure iliyoko mitaani kiuhalisia kwa wasanii hawa inafanya mada hiyo kutoepukika kirahisi.
Mtandao wa Bongo5 umeibua gumzo jingine baada ya kufanya mahojiano na promota wa muziki na filamu anaefanya kazi zake nchini Uingereza, Hadija Seif, maarufu kama Dida Fashion na alisema nchini humo Ali Kiba anapendwa zaidi ya Diamond.
Sio sasa hivi tu, tangu zamani to be honest kwa UK Alikiba yupo juu zaidi.  Sijui kwanini lakini kwa watu wenyewe ukisema labda kati ya Ali kiba na Diamond hapo nani aletwe, honestly watu wa UK yaani Ali kiba sijui aliwafanya nini lakini Alikiba UK is the best.” Alisema promota huyo.
Hata hivyo, ripoti hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti mashabiki wa muziki.
Mtu mmoja anaetumia jina la Blacksailors Jangombwe kwenye Facebook, yeye ni mtanzania anaeishi Uingereza ambaye alitofautiana na ripoti ya Dida

No comments:

Post a Comment