Monday, 22 September 2014

LICHA KUPEWA MATUMAINI, TEVEZ NJE KIKOSI CHA ARGENTINA KUIVAA BRAZIL!!

TEVEZ_IN_JUVEKOCHA mpya wa Argentina, Gerardo Martino, licha ya Wiki iliyopita kuleta matumaini kwamba Straika wa Juventus Carlos Tevez ataitwa kwenye Timu ya Taifa, lakini hakumchukua kwenye Kikosi chake cha kuivaa Brazil Mwezi ujao.
Jana Martino alitangaza Kikosi cha Wachezaji 19 na Tevez hakutajwa na huu ni mwendelezo wa kumtema Mchezaji huyo ambae amekuwa akiachwa tangu Mwaka 2011 Kocha aliepita Alejandro Sabella alipochukua madaraka na kujiuzulu baada ya Fainali za Kombe la Dunia hapo Julai 13 walipofungwa na Germany 1-0 kwenye Fainali.
Kati ya Miaka 2004 na 2011, Tevez aliichezea Argentina mara 64 na kufunga Bao 13.
Akiwa na Klabu yake Juventus, Timu aliyoisaidia kutwaa Ubingwa wa Italy, Tevez ameendelea kung’ara mno na Juzi aliifungia Bao wakati Juve inaichapa Malmo ya Sweden 2-0 kwenye Mechi ya Kundi A la UEFA CHAMPIONZ LIGI na pia Wikiendi kupiga Bao 1 na la ushindi wakati Juve inawachapa AC Milan 1-0.
Tevez, amewahi kuzichezea Klabu za Boca Juniors, Corinthians, West Ham, Man United na Man City, ana Miaka 30 hivi sasa na Wiki iliyopita Martino, ambae alitimuliwa na FC Barcelona kabla hajateuliwa na Argentina, alisema Tevez atachukuliwa ila itabidi agombee Namba 9 na Straika wa Napoli Gonzalo Higuain na yule wa Manchester City Sergio Aguero.
Kikosi hiki cha Argentina kitacheza Mechi ya Kirafiki na Mahasimu wao Brazil huko Beijing, China hapo Oktoba 11 ndani ya Bird’s Nest Stadium.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Sergio Romero (Sampdoria/ITA) Nahuel Guzman (Tigres UANL)
MABEKI: Mateo Musacchio (Villarreal/ESP), Pablo Zabaleta (Manchester City/ENG), Martin Demichelis (Manchester City/ENG), Marcos Rojo (Manchester United/ENG), Santiago Vergini (Sunderland/ENG), Federico Fernandez (Swansea City/ENG)
VIUNGO: Javier Mascherano (Barcelona/ESP), Lucas Biglia (Lazio/ITA), Javier Pastore (Paris Saint-Germain/FRA), Roberto Pereyra (Juventus/ITA), Angel Di Maria (Manchester United/ENG), Erik Lamela (Tottenham Hotspur/ENG), Enzo Perez (Benfica/POR), Nicolas Gaitan (Benfica/POR)
MASTRAIKA: Lionel Messi (Barcelona/ESP), Sergio Agüero (Manchester City/ENG), Gonzalo Higuain (Napoli/ITA).

No comments:

Post a Comment