Sekeseke hilo kubwa na la aina yake lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Gesti ya White Paris iliyopo eneo la Kimara-Kona jijini Dar na kusababisha umati (inzi) kujazana na kufunga mtaa.
ILIKUWAJE WANAWAKE KWA WANAWAKE?
Habari zilidai kwamba Mama la Mama alihisi mumewe anachepuka hivyo aliamua kumfuatilia nyendo zake hasa kwenye kipengele cha matumizi ya simu.Ilisemekana kwamba, Mama la Mama alichukua laini ya simu ya mumewe alipokuwa akijiandaa kwenda kazini.
MWANAMKE AINGIA MKENGE
Habari zilizidi kunyetisha kuwa baada ya kubadili sauti alifanikiwa kumwingiza mwanamke huyo mkenge lakini hawara huyo akamuuliza kulikoni ‘baby’ sauti imebadilika ndipo akamjibu anaumwa.
Ilidaiwa kwamba, bila kufikiria mara mbili, hawara huyo alikurupuka, akafunga safari kwa kuwa aliahidiwa penzi na fedha za kujikimu.Ilisemekana kwamba baada ya makubaliano Mama la Mama alikwenda kwenye gesti hiyo na kulipia chumba kisha akamsubiri kimwana ambaye alikuwa akitokea eneo la Kigogo, Dar.
Habari zilitiririka kuwa baada ya kufika kwenye chumba alichoelekezwa ndani ya gesti hiyo alishangaa kukuta aliyemuita ni mwanamke mwenzake ambapo alijikuta akiishiwa nguvu na kupigwa na butwaa.
Wanahabari wetu wakiwa eneo la tukio, walimwona mrembo huyo akiwa amechanganyikiwa na hapo ndipo sekeseke likaanza na kujaza kadamnasa ndani na nje ya gesti.
KIPONDO
Mama la Mama alishuhudiwa akimbonda mwanamke huyo kwa madai kwamba amekuwa akimzuzua mumewe na kumfanya ashindwe kutulia kwenye ndoa.
Mama la Mama alishuhudiwa akimbonda mwanamke huyo kwa madai kwamba amekuwa akimzuzua mumewe na kumfanya ashindwe kutulia kwenye ndoa.
Baada ya sekeseke zito, hawara huyo aliogopa kutoka nje ya gesti akihofia kupokea kipigo kutoka kwa raia wenye hasira kali waliokuwa wamezagaa nje hivyo aliamua kukodi chumba kingine ambapo alizama chumbani kisha kujifungia kwa ndani na kulala.
Akiwa kwenye mishemishe zake bila kutambua lolote, mwanaume aliyesababisha wanawake hao kukutana aliendewa hewani na mkewe na alipoulizwa kama anamfahamu mwanamke aliyeitwa gesti alijibu kuwa aliwahi kuwasiliana naye walipokutana baa kwani ni baamedi.
Awali kabla ya kujifungia chumbani, hawara huyo alidai kuwa mume wa Mama la Mama ni mpenzi wake ambapo wamedumu kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa takribani mwezi mmoja.
Alisema kwamba kilichomtokea anamwachia Mungu kwani amedhalilika kupita maelezo.
Hadi gazeti hili linang’oa nanga eneo la tukio Mama la Mama alikuwa ameondoka eneo hilo huku hawara akiendelea kutandika usingizi chumbani.
No comments:
Post a Comment