Tuesday, 23 September 2014
alipa milioni 33 kuongezewa titi la tatu…
MWANAMKE aliyejitambulisha kwa jina la Jasmine Tridevil (siyo jina lake halisi) mwenye umri wa miaka 21 amedai kufanyiwa upasuaji na kuongezwa titi la tatu kupitia mahojiano aliyoyafanya redioni.
Jasmine ambaye ni raia wa Tampa jijini Florida nchini Marekani anayejishughulisha na utoaji huduma ya massage, alilipa kiasi cha dola za Kimarekani 20,000 sawa na milioni 33.4 za Tanzania kufanyiwa upasuaji huo.
Mwanamama huyo katika mahojiano na Real Radio 104.1 alidai kuwa ameamua kufanya hivyo ili asiwe na mvuto kwa wanaume maana hataki kuwa na mpenzi huku akipenda kuwa staa katika TV japo
alipoulizwa sababu ya kwa nini hataki kuwa na mwenza hakutaja sababu.
Takribani madaktari 50 walikataa kumfanyia upasuaji huo wakiogopa kuvunja miiko ya fani yao hivyo kumchukua miaka miwili kumpata daktari aliyekuwa tayari kufanya hivyo.
Kwa sasa mama huyo anarekodi video itakayoonesha changamoto anazokutana nazo akiwa mwanamke mwenye matiti matatu.
Mtaalam aliyemfanyia upasuaji ambaye hakutaka kutajwa jina lake alichukua tishu katika tumbo la mama huyo ili kutengeneza titi la tatu.
Jasmine amesambaza picha zake mpya akiwa katika vazi la bikini kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya upasuaji huo.
Mrembo huyo amedai kuwa amekanwa na mama yake mzazi pamoja na dada yake.
“Mama yangu alikimbia, hataki kuongea na mimi wala hataki dada yangu aongee na mimi baada ya kuongeza titi la tatu,” Alisema Tridevil
Mbali na furaha aliyonayo mrembo huyo, bado anadai titi lake la tatu halifanani na mengine. Tridevil analazimika pia kujitengenezea mavazi yake mwenyewe ambapo ananunua mavazi mawili ya kuogelea
kisha moja analikata ili kupata nguo itakayokaa kwenye titi lake la tatu.
Jokate,Irene Uwoya,Adam Kuambiana na JB wakutana kwenye filamu ya mikono salama…
Tarehe 25.09.2014 Filamu kali na yenye kusisimua “MIKONO SALAMA” Itaingia kwenye Soko la Filamu za kitanzania na kuanza kuuzwa.
Sio
Filamu ya kukosa kabisa kwani Humo ndani kuna waigizaji mashuhuri na
Magwiji ambao wameshirikia na Mastar kutoka pande zingine.Jokate Mwegelo
maarufu kama Kidoti ameshiriki ndani ya Filamu hii akiwa na
Gwiji Jacob Steven(JB),pia kuna kipande ambacho amecheza Marehemu Adamu
Kuambiana humu ndani,pia Kuna wasanii wengine kama Irene Uwoya na
Single Ntambalike.Kaa Tayari kuona Filamu nzuri na yakitanzania.
Mlela ampiga dongo Nora
Mke amshushia kichapo ‘hevi’ hawara wa mume wake….!!
Sekeseke hilo kubwa na la aina yake lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Gesti ya White Paris iliyopo eneo la Kimara-Kona jijini Dar na kusababisha umati (inzi) kujazana na kufunga mtaa.
ILIKUWAJE WANAWAKE KWA WANAWAKE?
Habari zilidai kwamba Mama la Mama alihisi mumewe anachepuka hivyo aliamua kumfuatilia nyendo zake hasa kwenye kipengele cha matumizi ya simu.Ilisemekana kwamba, Mama la Mama alichukua laini ya simu ya mumewe alipokuwa akijiandaa kwenda kazini.
MWANAMKE AINGIA MKENGE
Habari zilizidi kunyetisha kuwa baada ya kubadili sauti alifanikiwa kumwingiza mwanamke huyo mkenge lakini hawara huyo akamuuliza kulikoni ‘baby’ sauti imebadilika ndipo akamjibu anaumwa.
Ilidaiwa kwamba, bila kufikiria mara mbili, hawara huyo alikurupuka, akafunga safari kwa kuwa aliahidiwa penzi na fedha za kujikimu.Ilisemekana kwamba baada ya makubaliano Mama la Mama alikwenda kwenye gesti hiyo na kulipia chumba kisha akamsubiri kimwana ambaye alikuwa akitokea eneo la Kigogo, Dar.
Habari zilitiririka kuwa baada ya kufika kwenye chumba alichoelekezwa ndani ya gesti hiyo alishangaa kukuta aliyemuita ni mwanamke mwenzake ambapo alijikuta akiishiwa nguvu na kupigwa na butwaa.
Wanahabari wetu wakiwa eneo la tukio, walimwona mrembo huyo akiwa amechanganyikiwa na hapo ndipo sekeseke likaanza na kujaza kadamnasa ndani na nje ya gesti.
KIPONDO
Mama la Mama alishuhudiwa akimbonda mwanamke huyo kwa madai kwamba amekuwa akimzuzua mumewe na kumfanya ashindwe kutulia kwenye ndoa.
Mama la Mama alishuhudiwa akimbonda mwanamke huyo kwa madai kwamba amekuwa akimzuzua mumewe na kumfanya ashindwe kutulia kwenye ndoa.
Baada ya sekeseke zito, hawara huyo aliogopa kutoka nje ya gesti akihofia kupokea kipigo kutoka kwa raia wenye hasira kali waliokuwa wamezagaa nje hivyo aliamua kukodi chumba kingine ambapo alizama chumbani kisha kujifungia kwa ndani na kulala.
Akiwa kwenye mishemishe zake bila kutambua lolote, mwanaume aliyesababisha wanawake hao kukutana aliendewa hewani na mkewe na alipoulizwa kama anamfahamu mwanamke aliyeitwa gesti alijibu kuwa aliwahi kuwasiliana naye walipokutana baa kwani ni baamedi.
Awali kabla ya kujifungia chumbani, hawara huyo alidai kuwa mume wa Mama la Mama ni mpenzi wake ambapo wamedumu kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa takribani mwezi mmoja.
Alisema kwamba kilichomtokea anamwachia Mungu kwani amedhalilika kupita maelezo.
Hadi gazeti hili linang’oa nanga eneo la tukio Mama la Mama alikuwa ameondoka eneo hilo huku hawara akiendelea kutandika usingizi chumbani.
Huyu ndio msanii staa wa kimataifa anaekuja Fiesta Dar 2014.
Wakati Tour ya Fiesta ikiwa inazunguka kwenye mikoa mbalimbali Tanzania ambapo weekend hii ni Mbeya na Songea, ametangazwa msanii wa kimataifa ambae ni rasmi atapanda kwenye stage ya Fiesta Dar es salaam October 2014 Leaders Club Kinondoni.
Rapper T.I ndio msanii wa kimataifa kwenye stage ya Fiesta October 18 2014 akiwa ni mkali ambae kwa sasa anamiliki chati za muziki kwa single yake ya No Mediocre
CAPITAL ONE CUP: ‘WATAKATIFU’ WAITAKATISHA ARSENAL EMIRATES, LIVERPOOL YAITOA BORO MATUTA 14-13!
CAPITAL ONE CUP – RAUNDI YA TATU
MATOKEO:
Jumanne Septemba 23
Arsenal 1 Southampton 2
Cardiff 0 Bournemouth 3
Derby 2 Reading 0
Leyton Orient 0 Sheffield United 1
Liverpool 1 Middlesbrough 1 [Baada ya Dakika 120, 2-2, Penati 14-13]
MK Dons 2 Bradford 0
Shrewsbury 1 Norwich 0
Sunderland 1 Stoke 2
Swansea 3 Everton 0
Fulham 2 Doncaster 1
+++++++++++++++++++++++
ARSENAL 1 SOUTHAMPTON 2
Wakiwa
kwao Emirates, Arsenal wametupwa nje ya Kombe la Ligi, CAPITAL ONE CUP,
na Southampton iliyotoka nyuma kwa Bao 1-0 na kushinda 2-1.
Alexis Sanchez alitangulia kuipa Bao Arsenal Dakika ya 14 kwa frikiki safi na Southampton walisawazisha baada ya Tomas Rosicky kumwangusha Sadio Mane na Dusan Tadic kufunga Penati hiyo katika Dakika ya 20.
Southampton walipata Bao lao la Pili Dakika ya 40 wakati Fulbeki wao wa Kulia Nathaniel Clyne alipounasa Mpira wa Kona uliokolewa akiwa Mita 35 na kuachia Shuti lililotinga wavuni.
Hadi mwisho Arsenal 1 Southampton 2.
VIKOSI:
Arsenal: Ospina, Bellerin, Chambers, Hayden, Coquelin, Rosicky, Diaby, Wilshere, Alexis, Campbell, Podolski
Akiba: Gibbs, Mertesacker, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Martinez, Ajayi, Akpom
Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Gardos, Targett, Wanyama, Schneiderlin, S. Davis, Tadic, Mane, Pelle
Akiba: Davis, Long, Cork, Bertrand, Mayuka, Reed, McCarthy
Refa: Keith Stroud
+++++++++++++++++++++++
LIVERPOOL 2 MIDDLESBROUGH 2
Hadi Dakika 90, Mechi hii iliyochezwa Anfield ilimalizika Bao 1-1 na kwenda Dakika za Nyongeza 30 ambazo Liverpool walipata ushindi wa Bao 2-1 kwa Bao la Dakika ya 109.
Liverpool walifunga Bao lao katika Dakika ya 10 baada ya Kipa wa Boro, Jamal Blackman, kuokoa Shuti la Rickie Lambert na Mpira kutua kwa Kijana wa Miaka 17, Jordan Rossiter, akiwa Mita 30 toka Golini na kupiga Shuti lililotinga wavuni.
Hadi Mapumziko Liverpool 1 Boro 0.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 62, Adam Reach aliisawazishia Boro kwa Bao laini la Kichwa.
Hadi Dakika 90, ngoma ilikuwa Sare ya 1-1 na Dakika za Nyongeza 30 zikaendelea na Liverpool kufunga Bao la Pili katika Dakika ya 109 kupitia Jesus Fernandez Suso.
Hata hivyo, katika Dakika ya 123, Raheem Sterling alifanya kosa kubwa kwa kutaka kuwarudishia Mabeki wake Mpira ambao ulinaswa na Bamford alieingia ndani ya Boksi na kuangshwa na Touré na Refa Jones kutoa Penati iliyofungwa na Bamford na Gemu kuwa 2-2.
Ikafuatia Tombola ya Mikwaju ya Penati ambazo Liverpool walikosa moja ile ya Raheem Sterling na Boro moja, iliyopigwa na Bamford, na Wachezaji waliobakia wote kupiga Penati, pamoja na Makipa wao na kufunga na Gemu kuwa Penati 10-10.
Ndipo Wachezaji wakarudia tena kupiga ambapo Balotelli aliifungia tena Liverpool na Bamford kufunga safari hii baada ya kukosa ya kwanza na kuendelea hadi Liverpool wakiongoza Penati 14-13 ndipo Albert Adomah alipopiga nje na kuwapa ushindi Liverpool kwa Penati 14-13.
VIKOSI:
Liverpool: Mignolet; Toure, Enrique, Sakho, Manquillo; Lucas, Rossiter, Lallana: Markovic, Sterling, Lambert.
Akiba: Jones, Moreno, Borini, Fernández Saez, Skrtel, Balotelli, Williams
Middlesbrough: Blackman; Fredericks, Ayala, Omeruo, Friend; Adomah, Leadbitter, Clayton, Reach; Tomlin, Kike.
Akiba: Gibson, Konstantopoulos, Husband, Vossen, Bamford, Nsue Lopez , Wildschut

Subscribe to:
Comments (Atom)