Pichani ni kulia ni Msanii wa bongofleva AbdulKiba akiimba sambamba na kaka yake Alli Kiba ambaye amekuwa akifanya vyema katika anga ya muziki wa kizazi kipya kupitia nyimbo zake mbili alizoziachai hivi karibuni,ikiwemo MwanaDaisalama na Kimasomaso,
Mkali mwingine wa muziki wa hip hop nchini Tanzania,Fid Q akiwashushia mistari wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta 2014,ndani ya uwanja wa Jamhuri usku wa kumkia leo.
Msanii wa bongofleva kutoka kampuni ya No Fake Zone Lina Sanga akiimba wimbo wake wa Ole Temba ambao umepokelewa vyema na mashabiki wake,ndani ya tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Sehemu ya umati wa watu waliofika kushuhudia tamasha la Fiesta 2014 ndani ya uwanja wa Jamhuri usiku wa kuamkia leo mkoani Dodoma.
Shangwe za mashabiki zikiwa zimetawala uwanjani hapo







No comments:
Post a Comment